Rais John Magufuli, leo anapokea taarifa ya kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu imesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki ndiye atawasilisha taarifa hiyo kwa Rais.
Kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma iliendeshwa na Serikali kuanzia Oktoba mwaka jana.
TAZAMA LIVE HAPA:
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini