Meneja wake, Jahz Zamba, alieleza kuwa, Mzee Damian amefariki dunia baada ya kugongwa na boda boda iliyokuwa kwenye mwendo mkali huko mjini Morogoro alikokuwa akiishi.
Alivunja mguu mmoja pale pale na kujeruhiwa vibaya kabla ya kupelekwa hospitali. Dereva wa boda boda naye aliumia vibaya ikiwemo kuvunjika taya na kujeruhiwa kichwa.
Jahz alisema baada ya Mzee Damian kupelekwa hospitali na kuwekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahtuti, kuna dawa zilikuwa zikihitajika lakini zilikosekana kwenye hospitali hiyo.
Ni pengo kubwa kwa Belle 9 kumpoteza baba yake, kwakuwa mara nyingi amekua akidai baba yake ni mwalimu muhimu katika maisha yake. Muimbaji huyo anayetokea Morogoro alimtaja mzazi wake huyo kuwa ni mtu anayemuinspire kwa mambo mengi.
Tunampa pole Belle kwa msiba huu mzito na Mungu ailaze roho ya baba yake mahala pema peponi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini