Habari hizo ni pigo kubwa kwa United inayopigania taji dogo la Ulaya, Europa League na kumaliza ndani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Nyota wa Sweden, Ibrahimovic amefunga mabao 28 katika msimu wake wa kwanza kwenye soka ya England wakati Rojo amefanikiwa kuwa beki wa kati chaguo la kwanza mbele ya kocha Mreno, Jose Mourinho.
Taarifa ya klabu leo Jumamosi imesema kwamba uchunguzi wa kina juu ya maumivu ya Marcos Rojo na Zlatan Ibrahimovic katika mchezo wa Europa League Alhamisi umethibitisha maumivu ya goti waliyopata wachezaji wote ni makubwa na watakuwa nje kwa muda mrefu.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini