Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mbunge Hussein Bashe atumiwa ujumbe wa Vitisho, Usome hapa...

Mbunge wa Nzega Vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Hussein Mohamed Bashe amesema kuwa ametumiwa ujumbe wa vitisho na watu wasiojulikana wakisema kuwa watamfanyika kitu kibaya popote pale alipo.

Bashe ambaye yupo kwenye vikao vya bunge vinavyoendelea mjini Dodoma ameandika leo asubuhi kupitia akaunti yake ya Tiwtter kuwa, ametumiwa ujumbe huo uliosomeka, “Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.”

Kufuatia vitisho hivyo, Mbunge Hussein Bashe amelitaka Bunge na Serikali kutofumbia macho vitendo hivi vya wananchi kutekwa na watu wasiojulikana.

Vitisho hivi kwa mbunge huyo vimekuja ikiwa ni siku chache tu tangu mwanamuziki Roma Mkatoliki na wenzake watatu walipotekwa na watu wasiofahamika wakiwa katika studio za Tongwe Records jijini Dar es Salaam.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017