Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mbunge wa Chadema Alazwa Ghafla Muhimbili, Afanyiwa Upasuaji

Wakuu salaam. Natumai tupo wazima. Kama inavyozunguka mitandaoni kuhusu kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Mhe. John Heche, taarifa hiyo ni ya kweli. 

Mhe. Heche alifika Hospitali ya Taifa Muhimbili siku ya Jumanne wiki hii kwa uchunguzi wa afya yake, baada ya uchunguzi wa awali alishauriana na daktari wake na kukubaliana angerejea Hospitali baada ya wiki mbili kwa matibabu rasmi.
Hata hivyo jana usiku Mhe. Heche alipata maumivu makali ya ghafla tumboni na leo asubuhi alikimbizwa Hospitali Muhimbili na kufanyiwa upasuaji (specialised surgery).

Upasuaji umeenda vizuri na hali yake inaendelea vema sana. Mwenyekiti wa Taifa Mhe. Freeman Mbowe amemtembelea kumjulia hali. 

Salum Mwalim
Naibu Katibu Mkuu
CHADEMA 
Jumapili April 16, 2017

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017