Wazazi nchini Zimbabwe ambao hawawezi kugharimia karo ya shule wanaweza kupeleka mifugo wao kama mbuzi na kondoo kama malipo, waziri mmoja amesema.
Waziri wa elimu nchini Lazarus Dokora aliiambia gazeti la Sunday Mail kuwa itabidi shule zilegeze masharti yao ya kudai karo ya shule kutoka kwa wazazi, na pia kando na mifugo wanaweza kubali kupewa huduma na ujuzi kama malipo.
"Ikiwa kuna mwashi au mjenzi katika jamii, yeye yuapaswa kupewa ile nafasi ya kufanya kazi kama njia ya kulipa karo," gazeti lilimnukuu.
Kuna shule ambazo tayari zinakubali mifugo kama malipo, Sunday Mail linasema.
Hata hivyo afisa katika wizara hiyo alifafanua kwamba wazazi ambao wanaweza kulipia watoto wao karo kwa mifugo ni wale wa mashambani, lakini wazazi walioko mijini wanaweza kulipa kutumia njia nyingine kama vile kuifanyia shule kazi fulani.
Tangazo hilo lilitolewa baada ya Zimbabwe wiki jana kupendekeza watu waruhusiwe kutumia mifugo yao kama mbuzi, ng'ombe na kondoo kama rehani wanapochukua mikopo katika benki.
Katika sheria mpya iliyopelekwa bungeni wiki hii, wanaohitaji kuchukua mkopo wanaruhusiwa kuandikisha mali inazohamishika ikiwemo magari na mashine kama dhamana, ripoti ya BBC World Business ilisema.
Mitandao ya kijamii ilichukulia habari ya "mbuzi-kwa-karo" na kejeli na ucheshi.
Mwandishi Zimbabwe Tsitsi Dangarembga aliuliza katika mtandao wa kijamii, Twitter, "kama tungeambiwa mwaka wa 1970 kuwa tunapigania kutumiwa kwa ng'ombe na mbuzi kama pesa, tungekubali kupigania uhuru?"
Mmoja wa watumizi wa mtandao wa kijamii Twitter alisema - Ikizingatiwa kuwa sio wanyama wote waliozaliwa sawa - je "naweza pata kazi kama mkaguzi wa mbuzi?"
-Credit:BBC
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini