Mfanyibiashara mmoja wa Uchina anafanya kampeni za kula wadudu ili kuimarisha tabia za kula nchini humo.
Matilda Ho alizungumza katika mkutano wa Teknonoljia, utumbuizaji na mitindo kuhusu umuhimu wa kusambaza ujumbe wa chakula chenye afya.
Anaunga mkono vyakula ikiwemo vile vilivyo na protini kutoka kwa viwavi.
China ina tatizo la ukuwaji kutokana na kunenepe kupitia kiasi na ugonjwa wa kisukari.
''China ina asilimia 20 ya watu duniani lakini ni aslimia 7 pekee ya ardhi yake ilio na rutba'', alisema bi Ho.
Mtu mmoja kati ya raia wanne wa Uchina anaugua ugonjwa wa kisukari na mmoja kati ya watu wanne amenenepa kupita kiasi.
Bi Ho alianza kukabiliana na swala hilo kupitia soko la mtandao la wakulima ambalo sasa linatoa bidhaa 240 kutoka kwa walkulima 57.
Mtandao huo umepata wateja 40,000 tangu uzinduliwe miezi 18 iliopita.
''Nilitaka kutumia teknolojia ili kupunguza pengo lililopo kati ya wakulima na wanunuzi'', bi Ho aliambia BBC.
''Ni haki yako kujua kule chakula chako kinakotoka na kuwahamasisha wateja''.
Chakula hicho husambazwa kwa wateja kupitia magari ya kielektroniki na maboksi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini