Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Nay Wa Mitego Asalimu Amri Aomba Msamaha


Baada ya kuporomoshewa maneno ya kashfa kwenye mitandao na mzazi mwenzake kwa kushindwa kumtunza mtoto zaidi ya kumuweka tuu kwenye mitandao ya kijamii na kujisifu, Nay wa mitego amekiri kubadilika na kuanza kumuhudumia binti yake.


Nay wa Miteho leo Rapa kupitia ukurasa wake wa Instagram ameamua kuudhihirishia umma kuwa kuanzia sasa atakuwa baba mwema na ataanza kuwahudumia watoto wote kwani yeye ni kama kioo hivyo hana budi kutekeleza hayo.


Nay wa Mitego wiki iliyopita aliandamwa na matusi huku akitolewa maneno ya kashfa na mzazi mwenzake  ambaye ni muigizaji wa filamu bongo, Skyner Ally akimtaka kuwa asishoboke kum-'post' mtoto wao aitwae Munnie kwani yeye hana mchango wowote ule kwa mtoto huyo tena alienda mbali zaidi kwa kusema hajui  hata gharama za nguo za ndani za mtoto huyo.


“Si kwa kichambo kile jamaniiiiii huu...Jamani inatosha basi povu. Nitapeleka matumizi. Nawapenda sana awa watoto wanguu. Wasiopeleka matumizi ya watoto wapo “-ameandika rapa Nay wa Mitego.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017