Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(Tanapa) Paschal Shelutete amesema aliyeshambuliwa na Simba na kujeruhiwa vibaya ni mlinzi wa kambi ya watalii iliyopo Hifadhi za Taifa za Tarangire.
Shelutete alikanusha taarifa zinazogaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa aliyejeruhiwa ni Mwalimu wa Chuo cha Sinoni cha Kimara Temboni aliyekuwa na wanafunzi wake.
Alimtaja mlinzi huyo kuwa ni Kilopa Samweli Loyani (46)na alikuwa katika kambi ya Maramboy inayomilikiwa na kampuni binafsi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini