Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Trump Kupunguza Kodi Kwa Wafanyibiashara

Rais Donald Trump anatarajiwa kupendekeza kupunguza kiwango cha kodi wakati atakapotangaza mpango wake wa kodi baadaye.
Maafisa wa Ikulu ya Whitehouse wanasema kuwa tangazo hilo la siku ya Jumatano litapelekea kupungua pakubwa kwa kiwango cha kodi inayolipwa na wafanyibiashara kutoka asilimia 35 hadi asilimia 15.
Wana uchumi wanasema kuwa kupunguzwa kwa kodi kutaongeza trilioni za dola kwa upungufu uliopo katika kipindi cha muongo mmoja ujao.
Lakini waziri wa fedha Steven Muchin amesema kuwa mpango huo wa kodi utajilipa wenyewe wakati wa ukuwaji wa kiuchumi.
Mpango huo wa bwana Trump hautarajii kuweka mapendekezo ya kuongeza mapato.Image cap
Mpango uliojadiliwa wa kodi ya mipakani utakaoongeza ushuru katika bidhaa zinazoagizwa kutoka nje unaoungwa mkono na spika Paul Ryan hautakuwa katika mpango huo.
Ikulu ya Whitehouse pia ina mpango wa kupanua uangalizi wa watoto ambapo mwana wa Trump, Ivanka ana upendekeza.
Wanachama wa Democrat hawatarajiwi kuunga mkono mpango utakaoongeza deni la kitaifa.
Hiyo inamaanisha kwamba wanachama wa Republican wanaodhibiti bunge na seneti watalazimika kufanya kazi chini ya maelezo ya bajeti ambayo yanawaruhusu kuendelea bila wao.
''Rais Trump angependa kuona bunge la Congress linapitisha mabadiliko ya kodi katikati ya msimu wa vuli'', imesema ikulu ya Whitehouse.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017