Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Yanga Wamwaga Mboga, Simba Kubinua Sahani na Bakuli Kabisa

HAJI MANARA, MSEMAJI WA KLABU YA SIMBA.
klabu ya simba imeitaka kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji ya shirikisho la mpira wa miguu tanzania (tff) mpaka kufikia machi 24, 2017, iwe imeshatoa maamuzi waliyoyaweka kiporo, kinyume na hapo watachukua maamuzi magumu.
haji manara, mkuu wa idara ya habari na mawasiliano klabu ya simba sc amewaambia waandishi wa habari kuwa anashangazwa na watani wao wa jadi kushikia bango suala hilo ili hali likiwa haliwahusu.
manara,  amesema hawatishwi na wapinzani wao waliosema wanamwaga mboga kuhusiana na kupewa pointi 3 dhidi ya kagera sugar na sasa kama vipi wao watabutua sahani na bakuli wakose wote.
“juzi kiongozi mmoja wa yanga ameongea na vyombo vya habari na kuitishia tff kwamba wameenda takukuru na polisi kuomba wafanya uchunguzi juu ya maamuzi ya kamati ya saa 72, baadae tff wanaitisha kikao cha kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kupitia maamuzi yaliyotolewa na kamati ya saa 72,” amesema manara.
amesema mkwara wa yanga umewatisha sana tff na kuanza kufanya vitu ambavyo kimsingi vilikuwa vimeshaisha. tff inaonekana kuipendelea yanga kwa kila jambo.
aidha manara amesema, kamati hiyo ya sheria na wachezaji mpaka leo haijatoa maamuzi juu ya suala ya tambwe dhidi ya juuko? mwaka wa pili unamalizika,  banda kampika ngumi kavilla ndani ya wiki moja uamuzi umeshatolewa, hii kamati tunashindwa kuielewa?
kagera kukata rufaa dhidi ya simba ndani ya wiki wameshakaa kikao kupitia taarifa, huu ni upendeleo wa wazi kabisa na hawawezi kukubali tff kuwa inawabeba upande mmoja tu.



Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017