Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Afya: Haya Ndio Madhara Ya Kula Nyama Ya Kuku Wa Kisasa.

kutokana na uhitaji mkubwa sana wa kuku hasa mijini ambapo kuna watu wengi sana, kuku wa kienyeji wameshindwa kabisa kutosheleza hitaji la watu hao.

teknolojia mpya ambayo iko wazi kwa watu wote imekuja na kuku wa kisasa ambao hukua ndani ya muda mfupi sana kuliko kuku wa kawaida yaani kuku wa kienyeji.


kumekua kuna elimu zikitolewa kwamba nyama nyeupe yaani kuku, samaki na ndege ni salama sana kuliko nyama nyekundu kama ngombe, mbuzi na nguruwe...ni kweli kabisa kama ukiwala wanyama hawa wakiwa kwenye asilia yao lakini ulaji wa kuku wa kisasa una madhara makubwa zaidi kuliko kula ngombe na mbuzi ambao wana nyama nyekundu.
kulingana na watu wengi kula sana kuku hawa hasa mahotelini, kwenye vyakula vya haraka kama KFC na kadhalika basi leo ntawaletea madhara ya kuku hawa kama ifuatavyo.

saratani au kansa mbalimbali:
 kuku za kisasa zina kemikali nyingi sana mfano kemikali phip ambazo huweza kusababisha mtu kupata kansa mbalimbali ikiwemo tezi dume na kansa ya matiti, kansa hizi zikigunduliwa mapema unaweza kupona lakini zikichelewa kugunduliwa zinakuua.

lehemu au cholestrol:
kuku wa kisasa wana lehemu nyingi sana, hii ni kemikali ambayo ni moja ya vyanzo vikuu vya kuziba mishipa ya damu hasa ya moyo na kuleta magonjwa ya moyo.
tafiti zinaonyesha kuku hawa wana lehemu au cholestrol nyingi kuliko nyama za ngombe au mbuzi na mayai yao yana lehemu mara tatu zaidi ya nyama ya ngombe na mbuzi.

kuongezeka uzito: 
kuku wa kisasa wameonyesha kuongeza watu uzito zaidi kuliko kuku wa kienyeji kwani kuku hawa wanakua na nyama nyingi sana ambazo huwafanya watu wazile kwa uroho, hii huweza kusababisha magonjwa ya moyo, kisukari na kiharusi.kumbuka kuku hawa hawafanyi mazoezi yeyote tufauti na kuku wa kienyeji ambao hutembea sana.

huongeza sumu mwilini:
kuku hawa kama nilivyosema mwanzo hukuzwa kwa kemikali nyingi sana ambazo huwakuza mara tatu zaidi haraka kuliko kuku wa kawaida, sumu hizo ni chanzo ya magonjwa kama kansa, kusahau sana uzeeni kitaalamu kama alzhaimer disease, magonjwa ya mishipa ya fahamu na kadhalika.
magonjwa haya hushambulia sana wazee hasa nchi zilizoendelea kama marekani, ujerumani, uingereza na kadhalika sababu ya mfumo wao wa kula hauna vitu asilia kabisa.

huongeza usugu wa dawa za binadamu:
 kuku hawa hupewa vyakula vyenye dawa za antibayotiki ambazo huwasaidia wasiugue na kufa hata kwenye mazingira magumu, sasa dawa hizi huliwa na binadamu na kumfanya azizoee sasa ikitokea anapata ugonjwa dawa nyingi atakazokula zitakataa kumtibu sababu mwili wake umeshazoea dawa.

mafua ya ndege:
mafua haya yameua watu wengi sana nchi zilizoendelea na kuwaacha wengi wagonjwa kitandani, avian flu ni moja ya magonjwa tishio ambayo husababisha viungo mbalimbali mwilini kushindwa kufanya kazi.

kukua haraka kwa watoto: 
daktari mmoja wa mifugo  kwenye chuo kikuu cha zambia ambaye amehusika sana na tafiti za kuku hawa anasema kwamba kuku hawa wanawekewa homoni za ukuaji kitaalamu kama growth hormone ili wakue haraka na madhara yake huathiri sana watoto ambao wanakua na kujikuta wanakua na kubalehe kabla ya wakati.

kuishiwa nguvu za kiume: 
sababu maini ya kuku ndio yanahifadhi sumu zote za mwili wa kiumbe chochote, tafiti zinaonyesha ulaji wa maini wa kuku wa kisasa kunaweza kusababisha kuishiwa nguvu za kiume



Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017