Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Aga Khan Kufanya Upasuaji Kwa Whatsapp



Dar es Salaam. Madaktari wa Hospitali ya Aga Khan na Prince Aly Khan nchini India, wanatarajia kuboresha huduma za upasuaji wa mifupa na majeraha kwa kutumia mtandao wa What’sApp.

Teknolojia hiyo mpya inatarajiwa kuanza kutumika nchini baada ya madaktari bingwa kutoka India kuwasili. Madaktari hao kutoka Hospitali ya Prince Aly Khan waliwasili nchini jana kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wenzao wa Hospitali ya Aga Khan kutumia teknolojia hiyo ya kisasa kufanya upasuaji.

Daktari bingwa wa upasuaji mifupa na majeraha wa Hospitali ya Aga Khan, Harry Matoyo amesema madaktari hao walioanza upasuaji wataondoka Jumatatu na kwamba, wanatarajia wataalamu wa hospitali hiyo watakuwa wamenufaika na uzoefu watakaopata.

“Tumetengeneza group (kundi) la What’sApp ambalo litatumiwa na madaktari bingwa wa upasuaji mifupa kati ya nchi hizi mbili, kwa ajili ya kusaidiana iwapo tutakwama wakati wa upasuaji. Tunaweza kupiga picha na kuuliza kitu kinachotakiwa kufanyika,” alisema Dk Matoyo.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017