Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Ahukumiwa Kwenda Jela Kwa Kuutusi Uislamu


Basuki Tjahaja Purnama anayejulikana kama Ahok ,alikuwa mkristo wa kwanza na raia wa Uchina kusimamia mji mkuu wa Indonesia na kesi hiyo ilionekana kuwa kipimo cha uvumilivu miongoni mwa dini tofauti nchini humo.
Alituhumiwa kwa kutusi Uislamu akitaja mstari mmoja katika Quran wakati wa kampeni.
Bwana Purnama alikana kukufuru mahakamani na akasema kuwa atakata rufaa.
Matamshi yake kuhusu Uislamu yalizua hisia kali miongoni mwa viongozi wa dini hiyo walio na msimamo mkali.
Walifanya maandamano ya mara kwa mara wakitaka ashitakiwe huku baadhi ya Waislamu wenye msimamo mkali wakitaka anyongwe.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa waandamanaji waliomuunga mkono na wale waliokuwa wakimpinga walitaka aachiliwe huru huku wengine wakitaka afungwe jela kwa muda mrefu.
Takriban maafisa 15,000 wa usalama kutoka maafisa wa polisi na jeshi wanaweka usalama katika eneo hilo huku maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia na magari ya kivita yakiyatawanya makundi hayo mawili.
Credit:BBC

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017