Kwa
wapita njia , kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Michigan,
alionekana ni mtu mzima akifurahia kuwapeleka watoto wake watatu katika
park, akiwa na mdogo wake Dominique.
Kitu
ambacho hakikuwa cha kawaida ni begi lake la kijivu alilolibeba
mgongoni muda wote, ndilo lililokuwa likimuweka hai. Ndani ya begi hilo
kulikuwa na mashine (power source) ya kusaidia kusukuma damu kwenye moyo
huo feki kifuani kwake.
Moyo
halisi wa Larkin ulitolewa kutoka mwilini mwake November 2014, na
kuwekewa kifaa ambacho kilimuzesha kukaa nyumbani badala ya hospitali,
wakati akisubiri kuwekewa moyo halisi wa binadamu.
Na
hatimaye mwezi Mei mwaka huu, Larkin anaendelea vema baada ya kuwekewa
moyo halisi wa binadamu katika kituo cha mishipa na moyo cha Frankel,
katika chuo kiku cha Michigan, na kutarajiwa kurudi nyumbani kwake
mapema ya wiki ijayo.
“Watu
wengi wangeogopa kwenda muda mrefu na moyo feki, lakini nataka
kuwaambia unatakiwa kwenda na woga, sikutaka kukubali upasuaji,
ilinichukua wiki mbili kukubali, kwa sababu inasaidia, naenda nyumbani
haraka baada ya upandikizaji, kwa sababu imenisaidia kuwa mwenye afya
hata kabla ya upandikizaji”, alisema Larkin.
Kwa
mujibu wa mtandao wa upandikizaji viungo (U.S. Organ Procurement and
Transplantation Network), takwimu zinaonyesha kuna takriban wagonjwa
4,000 duniani, wanaosubiri kupandikizwa moyo wa binadamu.
Kijana huyo kutoka nchini Marekani alitoa wito kwa watu kujitolea viungo mbali mbali, ili kuweza kuokoa maisha ya watu wengine.
Imetafsiriwa kutoka CNN.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini