Walikuwa wakitoka Turiani kwenda Morogoro ndipo basi hilo lilipogongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea Morogoro kwenda nchini Rwanda.
Morogoro. Watu 10 wamejeruhiwa na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Morogoro, watatu kati yao wakiwa na hali mbaya baada ya basi la kampuni ya Karim walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.
Walikuwa wakitoka Turiani kwenda Morogoro ndipo basi hilo lilipogongana uso kwa uso na lori lililokuwa likitokea Morogoro kwenda nchini Rwanda.
Walioshuhudia ajali hiyo walisema ilitokea saa sita mchana eneo la Ranchi ya Dakawa wakati dereva wa lori alipojaribu kuyapita magari mawili bila ya kuchukua tahadhari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema majeruhi walikuwa 24 na baada ya kufikishwa hospitali wengine walitibiwa na kuruhusiwa na waliolazwa ni 10, watatu wakiwa na hali mbaya.
Alisema dereva wa lori hilo anashikiliwa na polisi.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini