Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Ajali Ya Malori Kugongana Yaua Wawili Dar


Watu wawili wamepoteza maisha na mmoja kujeruhiwa kwa kuvunjika mguu baada ya malori mawili kugongana eneo la Tabata Relini, Dar, usiku wa kuamkia leo.


Imearifiwa kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo baada ya lori aina ya Fuso kuligonga lori jingine kwa nyuma hivyo kusababisha ajali na maafa hayo.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa, kwenye fuso kulikuwa na watu watatu ambapo wawili walifariki dunia papo hapo na mmoja ambaye ni dereva alivunjika mguu hivyo baada ya kuokolewa alikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Aidha Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wamewahi kufika eneo la tukio na kufanya uokozi.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017