Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Anusurika Kwenda Jela Kwa Kufanana Na Messi

Kufanana na Lionel Messi nusura kumpeleke jela mwanafunzi wa Kiirani baada ya kuzua vurugu kwa mashabiki waliotaka kupiga naye picha mitaani.

Mwanafunzi huyo, Reza Parastesh anayefanana na Messi aliwavutia mashabiki wengi wakiomba kupiga naye picha ‘selfies’ jambo lililosababisha vurugu na kulazimisha polisi kumkata na kumpeleka kituo cha polisi.

Pia, gari la Paratesh (25) liliongozwa na trafiki kutoka katika kituo hicho kutokana na mashabiki wengi wa Iran kuvutiwa naye.

Paratesh alisema: “Sasa watu wananiona mimi kama Messi wa Iran na wananitaka mimi nifanye kila kitu anachofanya. Ninapojitokea sehemu yoyote watu wote wanachanganyikiwa.

“Nina furaha sana kuona jinsi ninavyoweza kuwapa furaha watu wengi.”

Parastesh kwa sasa anabadilisha nywele zake na kufanana na Messi na mara kadhaa anapopita mitaani anavaa jezi ya Barcelona.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017