ASILIMIA
24.9 ya watanzania huvutishwa moshi wa tumbaku katika sehemu za kazi
hivyo kuchangia kuongezeka kwa wagonjwa wa saratani nyingi hapa nchini.
Hayo
yamebainishwa kwenye taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu inayohusu Maadhimisho
ya siku ya kutotumia tumbaku duniani.
“Hali hii isipodhibitiwa
vifo vitaongezeka kufikia asilimia 80 kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo
Tanzania na milioni 8 kwa mwaka duniani kote ifikapo 2030” iliongeza
taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa katika uchunguzi
uliofanywa mwaka 2013 na Wizaya ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia
Taasisi ya Utafiti wa Maradhi ya Binadamu(NIMR) wakishirikiana na
Shirika la Afya Duniani (WHO) ulionyesha asilimia 24.9 huvutishwa moshi
wa tumbaku sehemu za kazi, asilimia 14 ya watanzania hutumia tumbaku na
asilimia 17 ya watanzania hawavuti lakini wanavutishwa moshi wa tumbaku.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa tumbaku inaua watu takribani
milioni 6 kila mwaka na moshi wake huua zaidi ya watu laki 6 ambao sio
wavutaji wa tumbaku duniani .
Mbali na hayo Wizara ya afya
imedhamiria kupiga vita matumizi ya tumbaku kwa kuhakikisha hakuna
matangazo ya tumbaku kyupitia kwenye mabango
barabarani,luninga,redio,sinema,au kubandikwa ukutani na kwenye magari
ya matangazo.
Madhimisho ya Siku ya kutovuta Tumbaku
huadhimishwa Mei 31 kila mwaka duniani kote na kwa mwaka huu imebeba
kauli mbiu isemayo”TUMBAKU-TISHIO KWA MAENDELEO” .
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini