Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Bajeti ya Wizara ya Afya Yawasilishwa Leo Bungeni.......Waziri Ummy Aomba Kuidhinishiwa Sh. Trilioni 1

Bajeti ya Wizara ya Afya imewasilishwa bungeni leo na Waziri Ummy Mwalimu akisema kuwa malaria imeendelea kuwa changamoto nchini, licha ya kugawa vyandarua na kupulizia dawa katika mikoa mbalimbali.

Amegusia mambo mbalimbali ikiwemo  kuwataka wenye dalili za kifua kikuu wajitokeze kwa kuwa kinatibika.

"Wenye ukimwi kuanzia Juni wanapewa dawa za kupunguza makali bila kujali kupungua kwa CD4."

"Watoto 2020 wamefanyiwa upasuji wa vichwa vikubwa na mgongo wazi Muhimbili" Amesema Mwalimu

Pia amesema hudumu za kusafisha damu na figo zimeanza kupatikana katika hospitali za kanda. Amezilaani halmashauri zote ambazo hazikutoa fedha za mfuko wa maendeleo ya wamawake

Kuhusu mauaji ya wazee, Waziri Ummy amesema  yamepungua kutoka 190 mwaka 2015 hadi 134 mwaka 2016.

Waziri Ummy ametaja vipaumbele  vya wizara yake ambavyo ni  kuimarisha kinga na tiba, huduma za mama na watoto, upatijanaji wa dawa, kuimarisha vituo vya afya na hospitali, kuimarisha huduma lishe, matumizi ya tehama na kuongeza wanaotumia bima ya afya.

Ameeleza hakuna mjamzito atakayefariki kwa kukosa dawa ya kuzuia kifafa cha mimba na amesema zimetengwa Sh 7 bilioni kwa ajili yake.Amesema wajawazito 150,000 watapewa bima ya afya ili waweze kujifungua salama

Waziri Ummy amesema yeye si Daktari lakini ameshakuwa 'bush doctor' na ameomba Sh1,115,608,772,090.Fedha kwa ajili ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ni Sh37,906,880,090.Jumla ya fedha za fungu la Afya ni Sh1,077,701,892,000

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017