Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Chuo Cha Sokoine Kinanuka Ngono..Walimu Wajichukulia Vijana Wa Kiume Na Kike Kiulaini Kabisa


Ni wiki ya tatu sasa tangu taasisi ya Harakati Bora ilipowasilisha malalamiko kwa Uongozi wa Chuo kwa niaba ya wanafunzi wake 'wanaotumiwa vibaya' na waadhiri wao ikiwemo wanafunzi wa kike kutakwa kingono na waalimu kwa kutishiwa kufelishwa NA wanafunzi wa kiume kutumiwa kama 'makasuku' na walinzi wa waalimu kwa ahadi ya kusaidiwa kupata ajira baada ya masomo hayo. 

Chuo cha Sokoine-Kilimo kimekuwa hakikui kuendena na kasi ya mabadiliko katika sekta ya kilimo, teknolojia na kinazalisha wahitimu wasio na impact katika jamii kutokana na Elimu ya vitisho, ulaghai wa wahadhiri kwa wanafunzi. Chuo hiki kimegeuka genge la waalimu kupata 'mademu'.
Chuo cha Sokoine kina historia kubwa ya waalimu wake kuzaa na hata kuoana na wanafunzi wake. Hii ni aibu na tishio katika mustakabadh wa elimu Tanzania ikizingatiwa Chuo cha Sokoine ni chuo cha kilimo kikubwa Tanzania!

Ni lini mara ya mwisho taifa limevuna utaalamu, uvumbuzi au ubunifu kutoka kwa wanafunzi na wa chuo cha Sokoine? HAKUNA! na ni kwa sababu CHUO KINANUKA NGONO. 
Hata Ajira ktk chuo cha Sokoine zinatolewa kwa watoto wa Maproffesor waliodumu chuoni hapo. Na nitaleta mifano na ushahidi hapa jukwaani hivi karibuni.

8.May.2017 Uongozi wa Chuo uliwasilishiwa mashitaka juu ya mhadhiri George S.S Fasha anayetuhumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Sokoine kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi watatu kwa mpigo lakini hadi leo hii bado chuo kinafanya uchunguzi usio na dalili ya mwisho. 
Nimeambatanisha ushahidi wa mawasiliano kati ya Mkuu wa Idara Proff Damian Gabagambi na Idara ya HarakatiBora. Ikiwa taasisi hiyo imewasilisha malalamiko kwa niaba ya wanafunzi wake kwa Vice Chancellor wa chuo na utatuzi haujapatikana hadi leo hii. 

Sambamba na hayo, Mhadhiri George S. Fasha akishirikiana na mhadhiri mwenzake Marwa Raphael Masanda, wamekuwa wakiwatishia wanafunzi kutokusema ukweli na wakiwatafuta wanafunzi waliohusika katika kushitaki matendo yao. Hii inazidi kuwapa hofu wanafunzi wa Chuo cha Sokoine haswa katika hatma ya masomo yao na ufaulu katika mitihani.

Chanzo:Jf

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017