Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Diamond Aitaja Kazi Ambayo Hataki Mtoto Wake Wa Kike Aifanye


Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema kuwa angependa kumuona mtoto wake wa kiume, Nillan anakuwa msanii kama yeye lakini asingependa mwanae wa kike, Tiffa awe msanii.
Diamond alieleza sababu za kutotaka mtoto wake wa kike kuwa msaani kwamba anahofia sana wanaume kumtumia kwenye masuala ya kuajamiiana kutokana na yeye kuwa maarufu.
Diamond aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kupitia kipindi cha The Trend kinachoongozwa na Larry Madowo.
Mtu akishakuwa msanii, na idadi ya watu wanaomfahamu inaongezeka, hivyo wanaume wanaomtongoza nao wanaongezeka, kitu ambacho kitanitia presha kujua kwamba mwanangu ametembea na wanaume wengi, alisema Diamond
Mbali na wanae, Diamond pia alimsifia mzazi mwenzake, Zarinah Hassan na kusema ni mwanamke mwenye kujielewa sana, anayefahamu kuhusu kesho, na hivyo anamshukuru Mungu sana kwa kumpata na kumzalia watoto.

Unaweza kutazama mahojiano yote hapa chini.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017