Kahama. Baada ya kuzuiwa kuingia mgodini jana na kuamua kuweka ulinzi wa polisi kuhakikisha hakuna anayeingia wala kutoka, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack leo ametembelea mgodi huo na kupiga marufuku mgodi huo kuyeyusha wala kusafirisha dhahabu hadi kibali cha serikali.
Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kufanikiwa kuingia mgodini humo leo alfajiri, Mkuu huyo wa mkoa amesema shughuli hizo zitarejea baada ya serikali kupeleka Maofisa wapya wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini, TMAA kusimamia uzalishaji, ukaguzi na usafirishaji.
Katika hatua nyingine, uongozi wa mgodi wa Bulyanhulu kupitia kwa Meneja wake wa Ufanisi na Maendeleo ya Jamii, Elias Kasitila umetoa sababu za kiongozi huyo kushindwa kuingia kwenye eneo maalum la kuhifadhi dhahabu kuwa ni masuala ya kiulinzi kutokana milango yake kufunguka kwa muda wa saa 24, ulitegeshwa kufunguka saa 12:00 alfajiri leo.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini