Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Haya Hapa Mahojiano ya Nay wa Mitego na Polisi Kuhusu Wapo

Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
TAKRIBAN mwezi mmoja umekwishakatika tangu mkali wa michano ya Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ apate msukosuko wa kukamatwa na jeshi la polisi baada ya kuachia Wimbo wa Wapo, hapa amefunguka kwa mara ya kwanza maswali aliyoulizwa kituoni.
Pia msukosuko huo ulikuwa ni pamoja na wimbo wake huo kufungiwa na taasisi yenye dhamana na sanaa, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), lakini kutiwa mbaroni huko kulimfanya Nay kusikika sana kwenye vyombo vya habari Bongo. Hata hivyo, kifungo cha Basata hakikufi ka popote pale baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli  ‘JPM’ kukitengua wakati Nay mwenyewe akiwa katikati ya mahojiano na maafi sa wa jeshi la polisi.
Katika mahojiano haya, Nay anafunguka maswali aliyokuwa akiulizwa na maafande kuhusu maneno yaliyotumika kwenye wimbo huo, msikie
“Nilikuwa mtu kati, nikifafanua mistari niliyoimba kwenye wimbo wangu wa Wapo kuwa nilimaanisha nini. Sasa tukiendelea na mahojiano, maafi sa wa polisi walipokea simu kuwa, rais ameagiza niachiwe, mahojiano yakafi a hapohapo!” Tangu Nay atoke sentro hakupenda kabisa kufungukia lolote lile juu ya nini kilitokea sero zaidi ya kuwashukuru Watanzania kuwa naye katika kipindi hicho kigumu. Nay aliamua kufi cha pengine kwa sababu maalumu za usalama wake.
Hata hivyo, kiu ya watu wengi ilikuwa ni kufahamu angalau hata kwa kudodosa nini kilitokea akiwa na maafi sa wa polisi. Kufahamu alihojiwa nini, alisema nini ama alipigwa biti juu ya kuimba nyimbo zinazofi chua maovu kwa kutaja vitu waziwazi au la! Yote hayo mashabiki wa kazi zake na wapenzi wa burudani Bongo walipenda kuyafahamu, ambapo baada ya gazeti hili kumbana, mkali huyo ambaye ni gumzo kwa sasa mitaani mpaka bungeni ameweka wazi kila kitu ili kukata kiu ya watu wengi.
Amani: Sero umekaa siku ngapi?
Nay: Siku mbili. Nilikamatwa Jumamosi nikiwa Morogoro nikalala ndani, kesho yake nilisafi rishwa mpaka Dar, nikalala pia na kuachiwa siku iliyofuata ya Jumatatu.
Amani: Ukiwa sero ulikuwa katika hali gani?
Nay:Huwezi amini nilikuwa kawaida sana na nilikuwa sina wasiwasi hata kidogo. Kiukweli niliamini Mungu atanisaidia maana kwenye wimbo sikumtaja mtu. Pia nilifahamu hata kama ningepelekwa mahakamani ningeshinda kesi maana sikuwa na kosa lolote lile.
Amani: Baada ya kukamatwa mahojiano yako na maafi sa wa polisi yalihusu nini?
Nay: Yalihusu maneno yaliyotumika kwenye wimbo.
Amani: Kwamba?
Nay: Nifafanue mistari niliyokuwa nimeimba, majina ya watu au sehemu.
Amani: Uliulizwa kuhusu nini na nini?
Hebu funguka kidogo Nay!
Nay: Niliulizwa kuhusu jina la Bashite, nikasema Bashite ni jina maarufu kwa sasa nchini. Watu wanalitaja mitaani na lipo kwenye media. Nikaongeza kwamba, sijui ni la nani lakini nimeamua kulitumia kwa sababu ni maarufu na watu wanasema ni jipu jipya tena linatoka Koromije. “Niliwaambia kama kuna mtu anaitwa Bashite ambaye anahisi nimemdhihaki au kulitumia jina lake vibaya basi ajitokeze na anipeleke mahakamani.
“Pia wakaniuliza kuhusu Kolomije ni wapi? Nilieleza hata mimi nakusikia tu kutoka kwa watu na kwenye media kwamba ndiko anatoka Bashite. Lakini sikufahamu, sijawahi kufi ka na hata sifi kirii kama nitakuja niende. “Wakaniuliza kuhusu kichaa kupewa rungu? Nilisema kwamba, kichaa ni msamiati ambao upo muda mrefu mitaani. Kwamba, neno ‘kichaa’ linamaanisha mshikaji.
Kwenye wimbo wangu niliposema kichaa kapewa rungu na wanangu watanyooka, nilikuwa ninamaanisha ni juu ya washikaji wanaotoka kimaisha na kuwaburuza wenzao. “Kama wangebisha, nilichokuwa namaanisha ningewaambia waeleze wenyewe walivyoelewa. Au waniambie maana zao ambazo mimi sikuzimaanisha.”
Amani: Haya, kuna sehemu katika wimbo wako umeimba,’hee kuvamia ofi si za watu nayo ni kazi, wanangu pigeni kazi…’ hapa ulimaanisha nini na ulisema nini?
Nay: Hilo sikuulizwa. Amani: Hakuna kitu kingine ulichoulizwa?
Nay: Ni hayo tu maana mahojiano yenyewe hayakumalizika. Amani: Na vipi kuhusu kupigwa, kuchimbwa mkwara au vitisho vingine juu ya kuimba nyimbo za aina hiyo?
Nay: Sikupigwa wala kuchimbwa mkwara. Amani: Kipi ambacho huwezi kukisahau kipindi hicho?
Nay: Namna Watanzania bila kujali itikadi za vyama, dini, kabila na wala nyadhifa zao walivyojitokeza kunisaidia na kupaza sauti zao juu ya kilichokuwa kimetokea.
-GPL


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017