Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

INASIKITISHA:Mtoto Pekee Aliyenusurika Kifo Kwenye Ajali ya Karatu Aangua Kilio Baada ya Kuulizwa Swali


Jana Taifa la Tanzania lilikubwa na tukio kubwa la kusikitisha sana, wanafunzi zaidi ya 30 na walimu wawili walikufa katika ajali mbaya ya bus la shule iliyotokea Karatu Mkoani Arusha. Wanafunzi hao wa Shule ya Lucky Vincent School ya jijini Arusha walikuwa wanaenda mjini Karatu kwa ajili ya kufanya Mtihani wa Ujirani mwema na Shule ya Tumaini.

Katika ajali hiyo, wanafunzi wawili tu ndio wako hai, mmoja akiwa majeruhi na mwingine akitoka mzima wa afya hivyo vyanzo ya habari vilivyopo Hospitali ya Lutheran Karatu vinasema, jumla ya wanafunzi waliokufa inafika 38 japokuwa taarifa hizi hazijathibitishwa bado. Mmoja kati ya wanafunzi walionusurika, Ambaye hakuumia alihojiwa na Reporter wa Mawingu Tz kuzungumzia ajali ilivyokuwa lakini baada ya kupewa pole na kuulizwa swali, alianza kulia kwa uchungu kitendo kilichofanya mahojiano yashindikane…..Huku akilia na kwikwi juu alisema "siwezi kuongea siwezi…Mungu wangu, Mamaa". Hakika tukio hili linasikitisha sana, watanzania wanaomboleza na kila kona ya nchi hili tukio ndio gumzo.
Tuwaombee Mungu awalaze mahali pema peponi Malaika Hawa wasiokuwa na hatia. Comment RIP chini kwenye Comment tuendeleze sala za kuwaombea watoto hawa.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017