Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Kigwangalla: Upatikanaji Wa Dawa Nchini Umeimarika


 Serikali imesema kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini imeimarika na kufikia asilimia 83.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto Dk Hamis Kigwangalla alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo (Jumatano) mjini Dodoma.
“Moja ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano ni kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vya umma nchini,”amesema.
Kigwangalla amesema kuwa katika kutekeleza azma hiyo Serikali ilichukua juhudi za makusudi kwa kuongeza bajeti ya dawa kutoka Sh31 bilioni katika mwaka wa fedha 2015/16 hadi kufikia Sh251,500,000,000 bilioni katika mwaka wa fedha 2016/17.
Amesema hadi kufikia April mwaka huu jumla ya Sh112 bilioni zilikwisha kutolewa na kupelekwa Bohari ya Dawa (MSD) ili kuviwezesha vituo vya kutolewa huduma za afya vya umma kupata mahitaji ya dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi.
Waziri huyo amesema kufuatia ongezeko hilo la fedha kumbukumbu zinaonyesha kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini imeimarika.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017