MSANII wa maigizo ambae pia ni mwimbaji, Mussa Kitale amefichua siri inayomfanya aweze kumudu kuvaa vilivyo uhusika wa ‘teja’ katika uigizaji wake.
Akiongea nasi, Kitale alisema kuwa maisha yake yote toka utotoni amekulia uswahilini, Tandale na nyumbani kwao kulikuwa na kambi ya wahuni “mateja” hivyo alikuwa akiona maisha yao wanavyoishi.
“Sijawahi kutumia kilevi cha aina yoyote na sio muhuni, mimi ni mfuasi mzuri wa dini ya kiislamu pia ni mwalimu wa madrasa,” alisema Kitale. Alisema, ameamua kuigiza kama teja ili kubeba uhalisia, kufikisha ujumbe pamoja na kutoa elimu kuhusiana na ulevi huo hatari unaoharibu maisha ya vijana wengi nchini kwa sasa.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini