Maalim Seif tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini mwaka 1990 amegombea urais wa Zanzibar mara tano kupitia CUF na mara zote amekuwa akishindwa ingawa amekuwa akisisitiza kuwa anashinda lakini anaporwa ushindi.
“Inapofika wakati wa uchaguzi mkuu napata shinikizo kubwa la wananchi visiwani Zanzibara na bara wakitaka nigombee urais na wengine wanaamua kutoa pesa zao kunichukulia fomu ya urais,”alisema.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika mahojiano na kituo kimoja cha luninga, alisema mipango ya uchaguzi mkuu wa 2020 itaanza ndani ya chama baada ya kumalizika kwa kesi iliyopo mahakamani inayohusiana na mgogoro unaoendelea katika chama.
Maalim Seif amesema pamoja na kuwepo kwa mgogoro huo, hata hivyo hakuna mgawanyiko wowote wa wanachama uliojitokeza kiasi cha kufanya kuwa na makundi mawili kwa maana ya CUF Maalim Seif na Cuf Lipumba bali ipo CUF moja ambayo ni ya wanachama.
Kuhusu utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano, alisema yapo mambo mazuri yanayofanywa na Rais John Magufuli na yapo mengine yenye kasoro.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini