Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Majanga Yazidi Kuiandama Yanga ..engo Lao Mbio Kupigwa Mnada Kisa Madeni

JENGO la makao makuu ya Klabu ya Yanga lililoko makutano ya mtaa wa Jangwani na Twiga Kariakoo jijini Dar es Salaam, liko hatarini kupigwa mnada kutokana na deni la Sh. milioni 300 ambalo klabu hiyo inadaiwa, imefahamika.

Taarifa zilizopatikana jana jijini zinaeleza kuwa Kampuni ya Udalali ya Msolopa ndiyo imepewa mamlaka ya kusimamia mnada huo.

Akizungumza jana jioni, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alithibitisha kuwapo kwa deni hilo na kueleza kuwa uongozi umeanza utaratibu wa kulifanyia kazi suala hilo.

Mkwasa alisema kuwa deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo, lakini wanaamini watalilipa kabla ya mchakato huo wa kunadi jengo hilo la makao makuu haujafanyika.

"Ni kweli kesi iko katika Mahakama ya Ardhi na tumeshaanza kuifanyia kazi," alisema kwa kifupi Mkwasa, kocha na mchezaji wa zamani wa timu hiyo.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017