Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Mwenyekiti CCM Atajwa Kwenye Orodha Ya Wenye Vyeti Feki Wakati Hajasoma Kabisa

Matokeo ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma yameibua mapya mengine.
Hiyo inatokana na Mwenyekiti wa CCM wilayani Chamwino, Charles Ulanga kuhoji sababu za kutajwa katika orodha ya walioghushi vyeti vya kidato cha nne wakati hajawahi kusoma elimu ya sekondari.
Sakata la mwenyekiti huyo ni mwendelezo wa utata ulioibuka baada ya ripoti ya matokeo ya uhakiki huo ulioibaini wafanyakazi 9,932 wa Serikali na taasisi zake kuwa na vyeti vya kughushi, kutumia vya watu wengine au cheti kimoja kutumiwa na zaidi ya mtu mmoja.
Akizungumza na gazeti hili jana baada ya jina lake kuwa miongoni mwa wenye vyeti feki, Ulanga, ambaye pia ni Mratibu wa Elimu wa Kata ya Buigiri wilayani Chamwino mkoani Dodoma, alisema wakati wa uhakiki alipeleka cheti cha darasa la saba na cha ualimu daraja la tatu ‘A’.
“Nawashangaa wapi walipopata cheti cha kidato cha nne kwa sababu mimi nilipeleka vyeti viwili; cha darasa la saba na cha ualimu. Sasa hiki cha kidato cha nne walichokikuta feki sijui wamekitoa wapi?” alihoji Ulanga.
Credit:Mwananchi

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017