Maafisa wa Polisi katika jimbo la Bihar mashariki mwa India, wanasema kuwa panya wamebugia maelfu ya lita ya pombe, walionasa na kuhifadhi kituoni mwa polisi, ili kutumika kama ushahidi dhidi ya wagemaji.
Mwaka jana jimbo hilo lilipiga marufuku uuzaji na unywaji wa pombe. Na tangu wakati huo maafisa wa polisi wamenasa zaidi ya lita 900,000 ya pombe haramu.
Afisa mkuu wa polisi katika mji wa Patna, Manu Maharaj amesema kuwa, aliarifiwa na inspekta mkuu wa polisi hapo siku ya Jumanne kuwa, pombe hiyo yote imenywewa na panya.
Idara ya polisi sasa, imeamuru uchunguzi ufanywe kubaini madai hayo.
Waziri kiongozi wa jimbo la Bihar, Nitish Kumar, alitangaza kupiga marufuku unywaji, uundaji na uuzaji wa pombe, mara baada ya kuchukua hatamu za uongozi mwaka jana.
Inaonekana kama njia mojawepo ya kupunguza migogoro ya nyumbani, unyanyasaji na umaskini.
Mara kwa mara maafisa wa polisi hutekeleza operesheni ya ghafla kote katika jimbo hilo, ili kunasa pombe haramu. Polisi imewakamata maelfu ya watu na kunasa lita kadhaa ya pombe tangu sheria hiyo ianze kufanya kazi mwaka jana
Pia wamewatia mbaroni zaidi ya watu 40,000, kwa kuhifadhi pombe haramu manyumbani na madukani mwao.
Operesheni hiyo imechangia hifadhi kubwa mno ya chupa za pombe katika vituo vya polisi kama ushahidi.
Baadhi ya vutuo kadhaa vya polisi pia hukodi maghala ya kibinafsi ili kuhifadhi viwango hivyo vikubwa vya pombe.
Sheria inasema kwamba, yeyote anayepatikana akinywa au akiuza pombe, anaweza kufungwa jela jumla ya miaka 10.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini