Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Pogba Aanza Mfungo wa Ramadhani Akiwa Macca

taa wa Manchester United, Paul Pogba amesafiri hadi nchini Saudi Arabia, Macca ikiwa ni muda mfupi baada ya kuiwezesha timu yake hiyo kutwaa ubingwa wa Europa League.
Pogba amesafiri hadi nchini humo ikiwa ni mwanzo wa mfungo wa Ramadhani kwa waumini wa dini ya Kiislam.
Jumatano iliyopita, Pogba alifunga bao katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ajax katika fainali hiyo jijini Stockholm nchini Sweden.
Picha zimemuonyesha Pogba akiwa katika mavazi meupe sawa na waumini wengine.
Staa wa Manchester United, Paul Pogba akiwa nchini Saudi Arabia, Macca.
Bado haijajulikana mchezaji huyo atautumia muda wake wote wa mapumziko nchini humo au la.
Kabla ya kuondoka Manchester, aliweka video fupi akiwa na begi mtandaoni na kuandika: “Najiandaa kwenda kusema asante kwa kilichotokea msimu huu, tutaonana baadaye watu wa Manchester!”

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017