Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, jana aliishukuru familia yake kwa kumfariji wakati wa sakata la Faru John lililoitikisa wizara hiyo.
Profesa Maghembe alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa shukrani kwa wadau wa utalii wakati akimalizia kusoma bajeti yake, ambapo alitumia muda huo kumshukuru mkewe na familia yake.
“Namshukuru sana mke wangu, watoto wangu ambao walinifariji na mara zote walikuwa pamoja nami katika kutekeleza majukumu yangu hasa wakati wa sakata la Faru John,”alisema Profesa Maghembe.
Sakata la Faru John liliibuliwa mwaka jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa kwenye ziara Mamlaka ya Ngorongoro (NCAA), aliposema ana taarifa Faru John aliuzwa kwa Sh200 milioni.
Hata hivyo, Waziri mkuu alijulishwa kuwa Faru John hakuuzwa bali alipelekwa Gurmet kwa ajili ya kupanda Faru jike na kwamba alikufa kifo cha kawaida, lakini alidai aonyeshwe kaburi lake.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini