HAKUNA kitu ninachokichukia mwenzenu kama kusikia mtu anakula chakula kwa kuogopa, mpaka abembelezwe ndiyo apewe!! Hivi kwa nini unamkosesha raha mtoto wa mwenzio, kuku wako mwenyewe eti hadi umshikie manati, inahu! Mume huwezi kuishi naye kama kaka yako babu weee? Sipendi na sitaki kuona, kama una tabia hizi tena ukome na ukomae!
Ooh! Samahani hata salamu nimesahau kukujulieni, mu hali gani wapenzi wote wa kona hii, najua si akina mama pekee hata akina baba, kuna mtu mzima mmoja aliniambia akikosa kusoma kona hii hujisikia mgonjwa, full viungo vya mwili kumlegea kwa vile amepata mengi kupitia hapa.
Haya tuendelee na yetu hasa yaliyonifanya nifungue domo langu. Domo lisilo na breki, domo linalokuelimisha kama siyo kukuburudisha pia! Haloooooo eeehhh!
Kuna baadhi ya wanawake wenzangu wananiudhi sana kufi kia hatua ya kukosa raha, hivi unamuonea haya mumeo au mpenzio mkiwa ndani full khanga, full kulala na jinsi sipendi eeeh!
Nisikilize tena kwa makini nikupashe upashike mwanamke wee usiye na haya wala hila! Mwanamke ni pambo la nyumba, unatakiwa ujiachie mumeo akirudi mihangaikoni, mkilala vaa nguo nyepesi itakayomfanya asipepese mikono kukutafuta, upo?
Sa we endelea kuvaa mijinsi yako na mitisheti utafi kiri unaenda disko uone kama hajachepuka! Ndiyo, naongea na wewe unayenitolea macho kama fundi saa aliyesahau kurudishia nati huku mwenye saa anamsubiri!
Mwanamke anahitaji kuwa na machejo, siyo wengine ukifika muda wa kula kile chakula cha usiku utasikia; “Bwana mume wangu zima taa kwanza! Loo azime hiyo taa veepe! Kwani alikuoa gizani? Alipeleka mahari gizani?
Tena ushindwe na ulegee kama ulivyoshindwa kuishi maisha ya kufundwa! Yaani mwenzenu nakereka, utakuta mwingine ameshapitia mafunzo yote yale ya kike tunayofundwa, amefanyiwa hadi kicheni pati lakini likifika uwanjani linaingia kama gogo na minguo yake utafi kiri linakwenda vitani, unalo mbona!
Kwa taarifa yako tu, raha ya chakula kula bila kijiko, yaani siyo kuvaa minguo hiyo mizito tena ukumbuke umewekwa hapo ndani ili umtimizie mumeo anachohitaji.
Hebu nikuulize kwani mkila wote chakula cha usiku raha anapata nani? Si wote! Sa wee ukifi ka ule muda unajifanya eti una kaaibu, mara huwezi kula kwenye mwanga, huwezi kupiga vigelegele kama siyo na vifi jo, mwanamke gani wewe!
Mwanaume anatunzwa akatunzika mwanamke wee, anapambwa akapambika, anapikiwa chakula anakula atakavyo tena bilaya kijiko, anakuta kimepambwa vizuri.
Akirudi kazini amechoka, mfanye ajisikie vizuri!
Mwekee maji kabla ya kuoga na mfanyie japo masaji, siyo akirudi umekazana kutwa kwenye TV, ukitoka huko unahamia kwenye simu, wee wa kuchati chati na wewe hadi ukifi ka ule muda wa chakula cha usiku na minguo yako unaenda kulala, tukisema umerogwa mama wewe nitakuwa nakusingizia! Koma weee!
Kwa leo niishie hapa maana si kwa kushikwa na povu hili, mwenzenu lilikuwa limenifi ka haaapa! Tukutane tena wiki ijayo.
Ni mimi Shanging Mstaafu, Anti Nasra!
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini