Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Serikali Tupeni Ufafanuzi Kuhusu Shutuma Hizi Za Chama Cha Rais Uhuru Kenyatta Cha Jubilee

Chama cha Jubilee nchini kenya kimeishutumu serikali ya Tanzania kwa kuruhusu muungano wa NASA unaoongozwa na Raila Odinga kufungua kituo mbadala cha kuhesabia kura nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa jubilee , NASA baada ya kunyimwa ruhusa ya kuweka kituo hicho nchini kenya, wameoamua kukihamishia Tanzania, kikiwa na malengo ya kufanya ujumuishaji mbadala wa kura, lakini pia kudukua mifumo ya kuhesabu kura ya tume huru ya uchaguzi nchini kenya.



MY TAKE:
Serikali inabidi watoe ufafanuzi kama swla hili ni kweli au la.

Kuingilia uchaguzi na demokrasia ya nchi jirani kwa kuruhusu chama kimoja kutumia nchi yetu kufanya mambo yake ya kiuchaguzi ni kosa kubwa kidemokrasia na kidiplomasia.

lakini pia sisi wenyewe kama nchi hatuamini katika vyama kujijumlishia kura, ndo maana CHADEMA na kile kituo chao tuliwashughulikia, lakini pia Zanzibar uchaguzi ulihairishwa baada ya seif kujijumlishia kura na kutangaza matokeo kabla ya tume

Kama swala hili ni uongo, Jubilee na mwenyekiti wao ambaye ndo Rais wa sasa watuombe msamaha kama nchi kwa kutuingiza katika siasa zao za majitaka

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017