Kampuni ya SportPesa imeingia mkataba wa miaka mitano wa kuidhamini klabu ya Simba ukiwa na thamani ya Bilion 4.9 .
Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu nchini Kenya imeweza kuingia nchini Tanzania na kuja kufanya uwekezaji kwa klabu mbalimbali za mpira wa miguu.
Utiaji saini wa makubaliano ya mkataba huo umefanyika jioni hii katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na wadau mbalimbali wa mpira nchini.
Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva amesema mkataba huu utaweza kuwasaidia katika kuendelea kutoa hamasa kwa timu yao kufanya vizuri zaidi.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa SportPesa nchini Abbas Tarimba amesema kuwa wamefurahi sana kuingia mkataba na Timu ya Simba na mkataba wao utakuwa katika hatua tofauti kulingana na makubaliano waliyoyaingia.
Amesema kwa mwaka wa kwanza Klabu ya Simba watapata milioni 880 na katika miaka mitatu inayofuata watapata nyongeza ya asilimia 6 huku mwaka wa mwisho wa mkataba huo klabu hiyo itafaidika kwa kupata bilioni 1.08.
Mbali na hilo Tarimba amesema kuwa klabu ya Simba itafaidika kwa kupata fedha mbalimbali kama hamasa iwapo wataweza kupata ubingwa kwa kupewa bonus ya milioni 100 au kushiriki michuano ya kimataifa.
Kabla ya utiaji saini wa mkataba huo Simba iliweza kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya stand United magoli yakifungwa na Laudit Mavugo na Juma Luizio huku la Stand likifungwa na Kasim Selembe.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov akikabidhiana hati ya makubaliano ya mkataba na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva ukiwa ni mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov pamoja na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva wakisaini hati ya makubaliano ya mkataba na ukiwa ni mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania Abbas Tarimba
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini