Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiwa na viongozi wa juu wa SportPesa.
KAMPUNI ya SportPesa Tanzania leo imeahidi kutoa mchango wa Sh. Milioni 50 kwa ajili ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys ambayo ipo nchini Gabon kwa ajili ya kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Akitoa ahadi hiyo leo asubuhi katika uzinduzi wa kampuni hiyo uliofanyika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema kwamba wanatoa mchango wao wa Sh. Milioni 50 kwa ajili ya Serengeti Boys.
“Tumeamua kutoa mchango wetu wa Sh. Milioni 50 kwa timu yetu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys ambayo ipo nchini Gabon kwa sasa,”alisema Tarimba.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk.
Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas (kulia) akiwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati)
Viongozi wa SportPesa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mwakyembe
Harrison Mwakyembe alishukuru kwa mchango huo na akasema atahakikisha fedha hizo zinatumika vizuri kusaidia timu hiyo ifanye vizuri.
“Natoa shukrani zangu za dhati kwa mchango huu na ninaikaribisha sana kampuni ya SportPesa hapa Tanzania, na timu yetu kwa sasa tayari ipo Gabon, ni matarajio yetu itafanya vizuri na kufika hadi Kombe la Dunia,”alisema.
Mapema katika uzindzui wa kampuni hiyo inayoingia Tanzania baada ya mafanikio makubwa Kenya, Tarimba alisema wanataka kusaidia sekta ya michezo nchini.
Alisema SportPesa imefanikiwa kupeleka changamoto kubwa katika sekta ya michezo nchini Kenya kwenye michezo mbalimbali ikiwemo soka, raga, masumbwi na mbio za magari – na ikiwa kampuni yenye chimbuko barani Afrika, imefanikiwa pia kuwa mdhamini rasmi wa klabu ya Hull City ya Ligi Kuu England.
“Pia ni mshiriki rasmi wa michezo ya kubashiri kwa klabu kubwa katika Ligi Kuu ya England – Arsenal na Southampton ambao kupitia ushiriki huu wameweza kutoa mchango wa mafunzo mbalimbali kwa timu kubwa za mpira wa miguu nchini Kenya,”amesema Tarimba.
Tarimba, ambaye pia ni Mkurugenzi wa zamani wa Bodi ya Michezo Kubahatisha nchini, amesema wanatarajia kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya michezo Tanzania kupitia ushiriki na udhamini wao kwa timu za michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
“Kwa kuwa hii ni sehemu mojawapo ya maono ya SportPesa, Tanzania ina vijana wenye uwezo katika michezo mbalimbali na kupitia uwepo wetu nchini, tunadhamiria kutengeneza akina Mbwana Samatta na Hasheem Thabeet wengi sana, ambao watakwenda kutuwakilisha Watanzania kimataifa na kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa heshima kubwa sana,”amesema.
Tayari kuna ufununu, SportiPesa ipo kwenye taratibu za mwishoni za kuingia mikataba ya kuzidhamini klabu kongwe za soka nchini, Simba na Yanga – ingawa hilo Tarimba hakutaka kulizungumzia.
“Najua watu wana kiu ya kusikia kuhusu SportPesa kuzidhamini klabu kubwa za michezo Tanzania, lakini nawaomba wavute subira, wakati ukifika kila kitu kitawekwa hadharani,”alisema Tarimba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini