Shirikisho la Doka Duniani (FIFA) leo alhamisi ya Mei, 4 limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa soka Duniani kwa nchi Wanachama.
Katika orodha hiyo Tanzania imebaki katika nafasi yake ya 135 ambayo iliitwaa tangu mwezi Machi baada ya kushinda michezo yake miwili ya kirafiki ya kimataifa ambapo katika mchezo wa kwanza iliichapa Botswana mabao 2-0 kabla ya kuinyuka Burundi mabao 2-1 katika mchezo wake wa pili.
Nafasi ya kwanza ulimwenguni bado inashikiliwa na Brazil wakifuatiwa na Argentina‚ Germany‚ Chile na Colombia.
Kwa Afrika Misri bado wako kileleni,kidunia wako nafasi ya 19 wakifuatiwa na Senegal,Cameroon‚ Burkina Faso and Nigeria.
Duniani
1. Brazil (1)
2. Argentina (2)
3. Germany (3)
4. Chile (4)
5. Colombia (5)
6. France (6)
7. Belgium (7)
8. Portugal (8)
9. Switzerland (9)
10. Spain (10)
Afrika
19. Misri (19)
30. Senegal (30)
33. Cameroon (33)
35. Burkina Faso (35)
40. Nigeria (40)
41. DR Congo (41)
42. Tunisia (42)
45. Ghana (45)
48. Ivory Coast (48)
53. Morocco (53)
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini