Je unaujua mfuko mdogo katika suruali yako ya Jeans? Ndiyo, ule ambao umeshonwa juu kidogo ya mfuko mkubwa wa kulia.
Umewahi
hata mara moja kusimama na kujitafakari kwa nini huo mfuko mdogo mbele
ya suruali yako ya jeans upo hapo ulipo na nini hasa lengo la mfuko huo
zaidi ya pengine kudumbukiza sarafu au jojo ambayo unataka kuja
kuitafuna baadae au kuwaza kama ni fasheni tu katika nguo?
Kama
hujawahi kujiuliza hilo swali na bado hujui chanzo na lengo la mfuko
huo mdogo mbele ya suruali yako ya Jeans usijali kwani tovuti hii
itakueleza chanzo na lengo la mfuko huo.
Mfuko
huu ulikuwa unatekeleza jukumu muhimu sana miaka ya nyuma na ndio
sababu kubwa iliyopelekea watengenezaji wa suruali za Jeans kuweka mfuko
huo juu kidogo ya mfuko wa mbele wa suruali.
“Ni
mfuko maalum wa kuhifadhi saa. Ndiyo, inasemekana miaka ya nyuma ya
1,800, watu wengi walikuwa wanapenda kuvaa saa zao katika cheni na
kuzifungia katika viuno vyao. Ili kuweza kuweka salama saa zao
zisivunjike na kuharibika, Levi, watengenezaji wa kwanza kutengeneza
suruali za Jeans wakaamua kuweka mfuko huo mdogo mahali ambapo watu hao
wangeweza kuhifadhi saa zao salama na kwa wepesi zaidi.
Hivyo
ulianza kama mfuko wa kuhifadhi salama saa za mifukoni, japo baadae
ukaanza kupata matumizi mengine kama kuhifadhia sarafu, tiketi za
safari, kondomu, na viberiti hasa kwa watumia sigara.
Tangu hapo suruali za Jeans za aina zote zimekuwa zikitengezwa na mfuko huo mdogo bila kujali fasheni iliyopo kwa wakati huo.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini