Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Unaambiwa Hizi Ndio Dalili Za Mwanaume Anayekaribia Kupata Busha

kunapokuwa na
mkusanyiko wa maji kati ya tabaka mbili
za utando unaozunguka korodani. Kwa
hapa nchini ,
tatizo hili ni maarufu sana maeneo ya
mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi,
kiasi cha kuhusishwa na imani kadhaa
kama unywaji wa maji ya madafu. Aidha ,
tatizo hili limekuwa likichukuliwa na
baadhi ya watu kuwa ni hali ya
kudhalilisha ingawa kwa wengine
huonekana ni hali ya kuwa ‘ mzee wa
heshima ’ au ‘umwinyi ’.
Ifahamike pia kuwa , tatizo la mabusha
halitokei kwa wanaume watu wazima tu.
Watoto wa kiume hususani katika mwaka
wa kwanza (infants) pia ni waathirika
wakuu wa tatizo hili.
Kwa kawaida mabusha hayana maumivu
na wala hayaleti madhara , isipokuwa
kama
yatapata uambukizi kwa sababu nyingine
yeyote ile , hali inayowafanya wengi wa
waathirika , hasa wa mwambao, kuwa
wagumu kutafuta ufumbuzi wa tiba . Hata
hivyo, ni vyema kama mtu ana uvimbe
wowote kwenye pumbu zake, kutafuta
msaada wa kitabibu ili kuweza kuondoa
uwezekano wa kuwepo kwa magonjwa
mengine ya sehemu za siri kama vile
saratani ya
korodani (testicular cancer ) n. k .
Mabusha husababishwa na nini ?
Sababu za kutokea kwa mabusha
hutofautiana kati ya watoto wa kiume na
wanaume watu wazima .
Kwa watoto wa kiume mabusha huweza
kuanza kutokea kipindi wako tumboni
wakati wa ujauzito, korodani za mtoto wa
kiume huwa kwenye tumbo lake kabla ya
kushuka taratibu kuelekea kwenye
mapumbu . Wakati wa ushukaji huo ,
kifuko kinachozunguka korodani
kinachoitwa processus vaginalis hushuka
sambamba na kurodani hizo na
kufanya korodani kuzungukwa na maji .
Kwa kawaida , ndani ya muda wa mwaka
mmoja , kifuko hiki
hufunga na maji hayo yanayozunguka
korodani yote hufyonzwa na kurudishwa
kwenye tumbo la mtoto . Iwapo baada ya
kifuko kufunga na maji yaliyomo
kushindwa kufyonzwa kurudishwa
kwenye
tumbo la mtoto , mtoto hupata busha
lijulikanalo kitaalamu kama busha lisilo
na
mawasiliano (non - communicating
hydrocele ). Hali kadhalika, wakati
mwingine inawezekana kifuko
kikashindwa kufunga na hivyo maji
yakaendelea kujaa ndani ya kifuko
kuzunguka korodani.
Aina hii ya mabusha kwa watoto
ujulikana kama busha lenye mawasiliano
(communicating hydrocele ).
Kwa wanaume watu wazima Kwa
wanaume watu wazima , mabusha
husababishwa na
mambo makuu mawili;
1 .Kwanza , kitendo chochote
kinachochochea tando zinazozunguka
korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko
kawaida ,
2 . pili ni kupungua kwa ufyonzaji wa maji
yanayozunguka korodani kwa sababu ya
kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of
scrotal lymphatic system ) au kuziba kwa
mishipa ya damu
inayosafirisha damu kutoka kwenye
pumbu kwenda sehemu nyingine za
mwili (blockage of scrotal venous system ).
3 . Ongezeko la uzalishaji wa maji
linaweza kutokana na
Maambukizi au /na majeraha katika
korodani (testicular
inflammation au orchitis) au maambukizi
katika mshipa ujulikanao kama
epididymis yanayoweza
kusababishwa na kifua kikuu
(tuberculosis ) cha
makende , au maambukizi
yanayosababishwa na vimelea wa filaria
(filariasis ) wanaosababishwa

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017