Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

VIDEO:“Aliyelazwa Muhimbili Siye Aliyechora Nembo Ya Taifa” – Familia


Ikiwa ni siku chache tangu taarifa ya mzee ambaye alidaiwa kubuni na kuchora Nembo ya Taifa kuripotiwa na Serikali kuamua kumpatia msaada wa matibabu, familia moja imeibuka na kudai mzee huyo anayetajwa kuhusika kubuni siyo, bali ni mzee wao na ameshafariki.
Serikali kupitia Wizara ya Afya iliamua kumsaidia kimatibabu mzee Francis Maige maarufu kama ‘Ngosha’ ambaye alilazwa Hospitali ya Amana na kuamua kumhamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo baada ya tukio hilo familia nyingine imeibuka na kudai kuwa mzee wao ambaye sasa ni marehemu ndiye mchoraji wa Nembo hiyo.
Ayo TV imekutana na familia hiyo ambayo imeamua kufunguka na kuelezea kila kitu ukiwepo ushahidi wa mzee wao kuchora Nembo hiyo.
“Ushahidi ambao tunao ni wale watu wa rika lake ndiyo walikuwa wanashuhudia kwamba yeye ndiye aliyechora.”Yehoshaphat Jeremiah Kabati (Mtoto wa tatu wa anayedaiwa kuchora Nembo ya Taifa)

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017