Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Video:Tazama Spika Wa Bunge Jobu Ndugai Atoa Tafsiri Ya Neno FALA Kama Ilivo Katika Kamusi

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai jana ameonyesha aliumizwa na kitendo cha Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mh. Halima Mdee kumwambia 'fala' bungeni na kusema hata kama mtu humpendi lakini si vyema kumtusi matusi.

Job Ndugai alisema hayo alipokuwa akitoa maana ya neno fala bungeni ambapo ilibidi arejee maana hiyo kwa kusoma kupitia kamusi ya Kiswahili ambayo ilitoa maana kuwa fala ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri.

"Kwa neno ambalo alilisema Halima Mdee humu ndani, kamati imeenda kwenye tafsiri ikachukua Kamusi kwa neno lile alilosema ambalo maana yake kwa yule unayemwambia 'Fala' ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri, ni mtu mpumbavu, ni mtu bwege, ni mtu mjinga, ni mtu bozi, ni gulagula. Ndiyo maana nikasema sisi Waafrika hata kama humpendi namna gani mwenzako huwezi kumfanyia hivyo" alisisitiza Job Ndugai



Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017