Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Wolper:Nimekoma Mambo ya Mapenzi,Wanaume Ni Waongo Sana


MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa, kwa sasa amekoma kujihusisha na mambo ya mapenzi hivyo hahitaji kusikia suala hilo.
Akichonga na Showbiz XtraWolper ambaye hivi karibuni aliripotiwa kumpiga chini Harmonize aliweka wazi kuwa, kwa sasa hayupo kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa madai kuwa, wanaume wengi aliojihusisha nao hawakuwa wakweli, jambo lililomfanya ajiweke mbali na masuala hayo.

“Sihitaji kabisa kusikia suala linaloitwa mapenzi maana nimekoma, ninahitaji kufanya mambo yangu mengine kabisa hasa biashara na muvi,” alisema Wolper.


Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017