Mbunge wa Kigoma mjini kupitia tiketi ya ACT, Zitto Kabwe ameukosoa mpango wa serikali kuanza kujenga reli ya kati baina ya Dar es Salaam na Morogoro na kusema serikali inapaswa kuangalia vipaumbele vya maeneo ambayo shughuli za reli hiyo itasaidia
Zitto amebainisha hayo wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika mkutano wa Bunge Jijini Dodoma kwa kumtaka Waziri Profesa Makame Mbarawa aangalie takwimu ni wapi anapaswa apeleke reli ili aweze kupata pesa ya kujenga reli nyingine.
"Toka mwaka jana tumelalamika kuhusu jambo hili...Nawashukuru wabunge wemametoa tafsiri mpya ya reli ya kati, reli ya kati tafsiri yake ni Kigoma Dar es salaam au Dar es salaam Kigoma maeneo mengine yote ni matawi ya reli ya kati......
"Lakini ujenzi wa 'Standard Gauge' kwa hatua hizo wanazoziita za awali unatoka Dar es salaam kwenda Mwanza....Namuomba Waziri aangalie takwimu ni wapi atapeleka reli ili apate pesa ya kujenga reli nyingine.......
"Takwimu zinaonesha kwamba mizigo ambayo Tanzania inahudumia kwa nchi za maziwa makuu ni tani Milioni tano kwa mwaka kwa mujibu taarifa ya hali ya uchumi mwaka 2015/2016.
"Katika hizo asilimia 34 ni Zambia, asilimia 34 ni Kongo, asilimia 12 Rwanda, aslimia 6 Burundi, asilimia 2.6 Uganda...
"Unapoanza na 'Standard Gauge' matailion ya fedha ukaipeleka Isaka na Mwanza maana yake ni kwamba unaenda kuhudumia mizigo aslimia 15 ya mizigo yote tunayoipitisha unaacha kwenda kuhudumia mizigo asilimia 40 kwa maana ya Kongo na Burundi ambayo yote inapita Kigoma". Alisema Zitto
Aidha, Zitto amehoji wizara pamoja na serikali kuwa ni njia gani walizozitama mpaka kuamua kupeleka sehemu ambayo wanajua haiwezi kuleta faida kwa taifa.
"Economics' gani ambazo mmetumia katika kuhakikisha kwamba reli inaelekea mahali ambako hakuna mzigo..
"Sipendi kusema kwamba Kigoma inatengwa siyo lugha ambayo mimi kiongozi napenda kuzungumza lakini hili takwimu zote zinaonesha reli inapaswa kwenda kule ambako kuna faida, hampeleki kule ambako kuna faida ambako kuna faida hii maana yake nini ?...
"Lakini siyo hivyo tu Waziri, kuna fedha za Benki ya Dunia ...kwaajili ya ukarabati wa reli hata hizi Bilioni 200 za ukarabati wa reli ambao upo sahizi na zenyewe mmepeleka kule kule mnapopeleka 'Standard Gauge', mnashindwa hata kutudanganya kwa pipi". Alihoji Zitto
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini