Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Afungwa Miaka 23 Jela Kwa Wizi Wa Cheti Cha Kidato Cha Nne


Mahakama ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu kwenda jela miaka 23 mkazi wa Kijiji cha Kalovye, Osward Mpalasinge (26) baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja nyumba na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo cheti cha kidato cha nne.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Teotimus Swai baada ya mshtakiwa kukiri kosa na hivyo mahakama kumkuta na hatia pasipo shaka.
Kabla ya kusoma hukumu hiyo, mwendesha mashitaka, Baraka Hongoli aliiiambia mahakama kuwa, mshitakiwa alitenda makosa ya kuvunja na kuiba Mei 25 mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwa Veronica Crispin katika Kijiji cha Kalovye, Inyonga.
Aidha, Hongoli aliendelea kusema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuvnja nyumba hiyo aliiba nguo zenye thamani ya Sh 110,000 na cheti cha kidato cha nne cha Henreth Edward Kalamu, kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) mwaka 2015.
Mwendesha mashtaka huyo aliiomba mahakama kumpa mtuhumiwa huyo adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine kwani tabia za kuiba vyeti husababisha baadhi ya watu kupoteza kazi zao na hata wengine kufungwa.

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017