Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter

Aslay Ataja Mambo Matatu Ambayo Hato Sahau Yamoto Band


Msanii wa muziki Aslay anaye tamba na kibao cha  ‘Angekuona’  azungumzia mafanikio aliyoyapata akiwa na Bendi ya Yamoto ikiwa chini ya mkubwa Fella amesema ni mengi ila haya ni machache na yenye kipaumbele katika mafanikio yake kimuziki

Kutembea Nchi mbalimbali
“Yamoto bandi tumeweza kutembea sehemu mbalimbali hapa duniani jambo ambalo ni  neema kwa mwanamuziki kwakutengeneza Connection, tumezunguka marekani,Asia na Hata baadhi ya nchi za afrika kama vile Rwanda na kwingineko”

2.Kujengewa Nyumba

“Tumejengewa nyumba tukiwa yamoto bandi kila msanii anayumba yake ,hilo ni jambo kubwa sana kwani kuna baadhi ya watu wanafanyiwa management lakini hawapati  nafasi hiyo binafsi namshukuru sana Mkubwa Fella kwa kutufanya tuwe na makazi ”

3.Kuwa mimi kama mimi  na kujijenga zaidi

“Kwasasa ninamaisha yangu ambayo naweza kupata riziki za hapa napale  na ninaweza kuendesha familia yangu vizuri pasipo na shida na nimefanikiwa kufungua biashara ndogo ndogo ambazo zinaniingizia kipato cha kila siku”

Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka

===

Tupe Maoni Yako Hapa Chini
 

Mawingu Blog | Home Of Newz Copyright © 2017