Baba mzazi wa mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo, Urban Mwegelo amemfanya mwanadada huyo kuchanganyikiwa ‘kudata’ na kujikuta akiangua kilio kutokana na kuwa hoi kitandani akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
Chanzo makini kililiambia Wikienda kuwa, baba huyo ambaye hali yake ilikuwa mbaya siku kadhaa zilizopita, anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo jambo ambalo linamuumiza Jokate na kujikuta kila wakati akiwa na huzuni tu.
“Unajua Jokate anampenda sana baba yake ni kama rafiki yake kwa hiyo tangu aanze kuumwa amekuwa mwenye huzuni muda wote huku akiwaomba marafiki zake wa karibu wamuombee baba yake ili apone haraka na kurudi katika hali yake ya kawaida,” kilisema chanzo hicho.
Hivi karibuni Jokate aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter juu ya baba yake kuumwa ambapo aliwaomba mashabiki wake kumuombea katika kipindi kigumu anachopitia cha kumuuguza baba yake.
Baada ya kupata taarifa hizo, Wikienda lilimtafuta Jokate ambaye alikiri baba yake kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo na kwamba hali yake inaendelea vizuri kiasi.
“Baba yangu anaendelea salama tu, tunamshukuru Mungu kwa kweli siyo haba,” alisema Jokate bila kutaja hospitali aliyolazwa mzazi wake huyo.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini