Mwanamitindo na mfanyabishara kutoka nchini Kenya ‘Huddah Monroe’ amejisafisha mara baada ya vuguvugu la tuhuma za Diamond Platnumz kuhisi kuwa kuna kuzungukwa kwa mpenzi wake Zari TheBossLady.
Tuhuma hizo ambazo zilizua gumzo mtandaoni zilizima baada ya Zari kuanika ukweli wa picha iliyokuwa ikitumika katika tafsiri yenye utata. Baada ya hilo kupitia mtandao Huddah ajitenga kabisa kuwahi kuhusika kimapenzi na mme wa mtu hata kwa mpenzi wa rafiki yake Zari yaani Diamond Platnumz.
Kupitia Snapcha Huddah aliweka picha yenye maelezo ya kuwa hajawahi kufanya kitendo cha kumzunguka Zari na kusema kuwa kwa taarifa yoyote yenye kumhusisha na mahusiano ya namna hiyo ifahamike kuwa ni uongo wenye nia ya kuharibia jina lake tu.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini