Alhadi Mussa Salum ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Jijini Dar es salaam, ameitoa kauli hiyo jana jioni katika hafla maalum ya Futari kwa wajumbe wa kamati hiyo iliyoandaliwa na uongozi wa Shia Ithnashariya Tanzania Kigogo Jijini humo.
Alhad Mussa alisema kuwa kumekuwepo makundi ya watu ambao wanabeza amani iliyopo nchini kwasasa, Nakuwapa neno kuwa kama wanahisi amani si mali kitu basi waombe dua vita ije, waone kama wataishi kwa raha waliyonayo sasa hivi.
Hata hivyo Alhadi Mussa alimaliza kwa kusema wataendea kuipigania kwa kuiombea Amani iliyopo usiku na mchana, na hivo hata watanzania bila kujali itikadi zao nao pia waipiganie na kuilinda kwa nguvu zote.
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini