MASTAA wa soka katika nchi zilizoendelea ni kawaida kuwa na mishahara mikubwa, hali ambayo inawafanya baadhi yao kuwa na maisha ya gharama kubwa.
Licha ya makato makubwa ya kodi lakini bado wengi wao wamejikuta wakiwa ni wapenzi wa kununua vitu vyenye gharama kubwa kwa kuwa wanalipwa mishahara mikubwa pia na muda wao mwingi wanautumia katika masuala ya soka, hivyo wanakosa nafasi ya kustarehe.
Moja ya vitu ambavyo vinapendwa na wachezaji wengi mastaa ni magari ya kifahari, wapo baadhi yao ambao wananunua ya kawaida lakini wengine kwao hiyo ndiyo starehe kubwa ya kuonyeshea.
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ni mmoja wa wachezaji wanaojulikana kwa kumiliki magari ya kifahari na vitu vingine, suala la kununua kisha kuonyeshea kwake ndiyo maisha yake.
Nyota wa Barcelona, Lionel Messi yeye pia anamiliki vitu vingi vya kifahari ikiwemo magari lakini siyo mtu wa kujionyesha.
Ronaldo ana magari mengi ambayo amewahi kumiliki na mengine bado ni mali yake yakiwemo Lamborghini, BMW, Bentley, Mercedes-Benz Sports Coupe, Porsche, Ferrari na Audi.
Gari yake yenye thamani kubwa ambayo amewahi kuonyesha mitandaoni ni Bugatti Veyron Grand Sport Vitesse ambayo gharama yake ni zaidi ya pauni milioni 1.8 (Sh bilioni 5)
Kutokana na kulipwa mshahara wa pauni 365,000 (Sh bilioni 1) kwa wiki, Mreno huo anao uwezo wa kununua magari mengi ndani ya mwezi mmoja yenye thamani kubwa.
Messi naye licha ya kuwa siyo mtu wa kujionyesha, anamiliki gari la thamani aina ya Ferrari F430 Spider lakini gharama yake siyo kubwa kama ile ya Ronaldo.
Ukifananisha mishahara wanayolipwa mastaa hao kwa wiki, unaweza kusema kuwa Messi anahitaji kucheza kwa dakika 31 na sekunde 32 tu aweze kupata fedha za kununua gari lake hilo aina ya Ferrari, wakati Ronaldo yeye anatakiwa kucheza kwa saa tano ili apate kiasi cha kununua Buggatti yake.
Upande wa pili ni kuwa kuna wachezaji kadhaa ambao licha ya kuwa na majina makubwa lakini wao wamekuwa wakinunua magari yenye thamani ya chini tofauti na ustaa wao.
Mfano ni aliyekuwa winga wa Manchester City, Jesus Navas ambaye anamiliki gari aina ya Nissan Micra ambalo thamani yake ni pauni 11,800 (Sh milioni 33).
Utafiti unaonyesha kuwa kwa mshahara ambao alikuwa akipata Man City, Navas anao uwezo wa kucheza kwa dakika 11 na sekunde 17 tu akapata kiasi cha fedha cha kununua gari hilo analomiliki.
Hiyo inamaana kwa dakika 90 za mchezo kamili anao uwezo wa kununua gari hizo nane.
Straika wa zamani wa Manchester United na Man City, Carlos Tevez ambaye yupo China akicheza, inaelezwa kuwa analipwa pauni 635,000 (Sh bilioni 1.8) kwa wiki.
Anaichezea Shanghai Shenhua na anamiliki gari aina ya Porsche Panamera Turbo S ambayo thamani yake ni pauni 115,100 (Sh milioni 326).
Kutokana na malipo ya mshahara wake, anaweza kununua gari la aina hiyo kila baada ya dakika 11 na sekunde 35 ambazo atakuwa uwanjani akicheza.
Kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante ambaye hana makeke katika maisha ya kawaida, anamiliki Mini Cooper SD ambalo ni gari lisilo na gharama kubwa.
Wanavyoweza kununua magari kwa viwango vya mishahara
Gari Muda wa kucheza
Navas Man City Nissan Micra 00:11:17
Carlos Tevez Shanghai Porsche Panamera Turbo S 00:11:35
Kante Chelsea Mini Cooper SD 00:12:58
Llorente Swansea Fiat Punto 00:13:52
Witsel Tianjin Cadillac Escalade 00:15:31
Howedes Schalke 05 VW Beetle Cabrio 00:15:52
Schurrle Dortmund Jeep Wrangler Sahara 00:18:37
Ighalo Yatai BMW X6 00:19:11
Buffon Juventus Fiat 500 00:19:48
Pelle Shandong Morgan Aero 8 00:19:58
Straika wa Shandong Luneng, Graziano Pelle anayecheza China, anamiliki gari la Morgan Aero 8, lenye thamani ya pauni 92,610 (Sh milioni 262), ambalo anaweza kulinunua akicheza kwa dakika 20 tu.
Kipa wa Juventus, Gianluigi Buffon anaendesha Fiat 500 ambalo anaweza kulinunua baada ya dakika 19 na sekunde 48.
Wanavyoweza kununua magari kwa viwango vya mishahara
Gari Muda wa kucheza
Messi Barcelona Ferrari F430 Spider 00:31:32
Rooney Man United Aston Martin Vanquish S 00:50:36
Ronaldo Real Madrid Bugatti Veyron Grand V 05:15:20
Gray Leicester Lamborghini Huracan 09:52:49
Boyd Burnley Mercedes 300 SL 45:40:23
Bonyeza HAPA Kudownload Applicationi Ya Mawingu Blog Kwenye Simu Yako Ili Kupata Habari Zetu Haraka
===
Tupe Maoni Yako Hapa Chini